Hii ni sehemu ndogo ya kitabu nilichoandika chenye kichwa,(Kusifu na kuabudu kwa udhihirisho wa Mungu). Karibu tusome kwa uponyaji wa kanisa.Barikiwa.
Nilikuwa nikiulizwa hili swali mara kwa mara nikiwa nikifundisha somo hili la kusifu na kuabudu kwa njia ya muziki hasa na vijana wa mashuleni na vyuoni, na swali hili linapokuwa linaulizwa hadhira inakuwa na shahuku sana kupata majibu kutoka kwangu, na mimi huwa sitoi majibu ila huwa natamani kusikia watu wengi wanasema nini juu ya hili la kusikiliza nyimbo za dunia(secular music) ya kuwa ni dhambi ama si dhambi. Sifahamu kwanini hizi nyimbo au muziki huu wakauita wa dunia, kwa lugha ya kiingereza wanasema "secular music", siitaji kwenda mbali sana kuitaji kujua kwanini waliita miziki ya dunia lakini nafikiri unaelewa mtu anaposema muziki wa dunia. Inawezekana huyu mtu alivyoita hivyo alifanya mahusiano kati ya dunia na mambo yanayofanyika na biblia inavyoelezea juu ya dunia, sifahamu na mimi nimelikuta hilo neno.
Unapolirudisha swali hili kwa unaowafundisha hapo ndipo utakapoona jinsi gani mungu wa dunia hii alivyowapofusha na kuwapotosha wakristo wengi ili wasitambue kweli na makusudi ya Mungu katika maisha yao, biblia inasema,
"Basi nasema neno hili, tena nashuhudia katika Bwana, tangu sasa msienende kama mataifa waenendavyo, katika ubatili wa nia zao,ambao akili zao zimetiwa giza,…",Waefeso 4:17-18.
watu wengi hasa wakristo wa kizazi cha sasa waibariki nyimbo na miziki ya dunia hii na shetani kuwadanganya kuwa hakuna shida yoyote unaposikiliza na kwamantiki hiyo wokovu wa sasa umerahisishwa na kuwa kama wokovu ni maisha ya kawaida suala ni kumkiri na kumpokea Yesu. Sikiliza mtu wa Mungu, kumpokea Kristo pekee hakusaidii wala hakukupi wewe tiketi ya kwenda mbinguni, utambue kwamba wokovu si kulikiri tu jina la Bwana Yesu bali kuyaishia maisha aliyoishi Kristo naye afanyike Bwana kwako na si mwokozi tu.,ndio maana utakuta watu wengi Yesu amebaki kuwa mwokozi wao hadi leo lakini si Bwana, kivipi? Yesu anapokuwa Bwana maana yake anatawala kila kitu katika maisha yako yaani,namna ya kuenenda,kuongea kuwaza na kutenda. Siitaji zaidi kuelezea kuhusu wokovu bali nahitaji upate muanga juu ya jambo hili ninalolizungumzia ili ufahahamu kuwa kama ni mshabiki basi unashangilia timu inayoshinda au inayoshindwa.
Paulo anawaambia Waefeso, "tangu sasa msienende kama mataifa waenendavyo". Unapozaliwa mara ya pili biblia inasema wewe ni kiumbe kipya, hiyo inamaana yote ambayo ulikuwa unayafanya kabla hujaokoka yanabadilika, unabadilika kuongea kwako, unabadilika kuvaa kwako, unabadilika kuwaza kwako, unabadilika katika usemi yaani huwezi tena kuwa na lugha ileile ya mwanzo na pia hata mavazi yako, hii nikiwa na maana uvai kitu chochote tu ilimladi kinaitwa nguo.
Hivyo ulivyo sasa ni matokeo ya, mambo yote ambayo ulikuwa ukisoma, mambo yote ambayo umekuwa ukitazama au kuangalia katika luninga(tv), marafiki wote ambao umekuwa ukiwa nao, chakula ambacho umekuwa ukitumia pamoja na yote ambayo umekuwa ukisikiliza na hayo ndiyo yanayomjenga mtu wa ndani zaidi na si wa nje. Wapo wakristo wengi ambao wamemkiri Kristo kuwa Bwana lakini bado wanasikiliza nyimbo ambazo mataifa wanasikiliza na kwasababu wanasikiliza na si kusikia basi hayo wanayoyasikiliza ndiyo ambayo yanarudisha nyuma maisha yao ya kiroho, kwasababu hayapo katika msingi wa neno. Ninaweza kukupa mfano wa waimbaji wachache ambao wanakubalika na watu wengi duniani, na watu wengi wakiwemo wakristo waliookoka wakisikiliza nyimbo zao nakuzipenda na zingine zikitukana jina la Kristo Yesu. Kati ya watu hawa ukiangalia na kutazama maisha yao utaona kuwa kuna ibada ya shetani katika maisha yao na wala hutaitaji nyimbo zao.
Ngoja nikupe mfano wa wanamuziki wachache tu ambao nyimbo zao zimesikika lakini hazimtukuzi Mungu na utakuta mkristo aliyeokoka anazisikiliza na wakati mwingine kuziimba na mwishoni kucheza na baadae dhambi inadhihirishwa katika mwili baada ya kuitenda moyoni.
Huyu ni Frank Zappa mmoja wa waimbaji wa miziki ya dunia anasema "I'm the devil's advocate. We have our own worshippers who are called 'groupies.' Girls will give their bodies to musicians as you would give a sacrifice to a god." -Frank Zappa (Peters Brothers, What About Christian Rock, p. 17), "mimi ni mshabiki wa shetani. Tuna watu wetu wenyewe ambao wanafanya ibada au waabuduo ambao wanaitwa ' groupies.' Wasichana au wanawake wanatakiwa watoe miili yao kwa wanamuziki kama unavyootia sadaka kwa miungu."
Sikiliza Michael Jackson anachosema "My goal in life is to give to the world what I was lucky to receive . . . the ecstasy of divine union through my music and my dance." "lengo langu katika maisha ni kuupa ulimwengu kile kitu nilichobahatika kukipata…kuleta ushirika wa kiroho kwa njia ya nyimbo zangu na muziki wangu. (Mtu yeyote asikudanganye njia pekee ya kuleta ushirika mtakatifu ni kwa njia ya Yesu Kristo tu) Yohana 14:6.
Huyu hapa ni Bon Jovi anasema " . . . I'd kill my mother for rock and roll. I WOULD SELL MY SOUL." Tafsiri " nigemuua mama yangu kwasababu ya music wa rock and roll. NINGEUZA NAFSI YANGU" (Smash Hits magazine)
Embu msikilize huyu mwanamuziki mwingine anayeitwa Prince anachosema "When one finds himself, one finds God. You find God, and you find yourself." tafsiri, yeye anadai kuwa hakuna Mungu ila tu wewe mwenyewe waweza kuwa Mungu. je, hiki ndicho biblia inafundisha?
Huyu hapa ni John Lennon "Christianity will go, it will vanish and shrink. I needn't argue about that. I'm right and will be proved right. . . We're more popular than Jesus now." Tafsiri "Ukristo utapita, utapotea nakuyayuka. Wala sihitaji kubishana na mtu kuhusu hicho. Mimi nipo sahihi na sikuzote nitakuwa sahihi" (San Francisco Chronicle, April 13, 1966, p.26)
Huyu hapa ni Axl Rose wa bendi inayoitwa 'Guns N' Roses' anasema "I can't get enough of women. I have sex as often as possible...It's not easy to be in a one-on-one relationship if the other person is not going to allow me to be with other people." Tafsiri " Sitosheki na wanawake, kila mara ninafanya ngono pindi ninapohitaji……Sio rahisi kuwa katika mahusiano na mtu mmoja ambaye hata niruhusu kuwa na mahusiano na watu wengine.
Huyu hapa ni Madona anasema "Be strong, believe in freedom and in God, love yourself, understand your sexuality, have a sense of humor, masturbate, don't judge people by their religion, color or sexual habits, love life and your family." Tafsiri, " kuwa hodari, amini katika uhuru na Mungu. Jipende mwenyewe,tambua jinsia yako,uwe mcheshi, piga puli, usiwahukumu watu kwa dini zao, rangi au tabia za ngono,penda maisha na familia yako" . je,hivyo ndivyo neno la Mungu linavyotufundisha?
huyu naye pia ni kati ya wanamuziki waliokonga mioyo ya watu wengi na anasikilizwa na mamilioni ya watu ulimwenguni wakiwemo watu wanaoitwa wakristo. moja kati ya nyimbo zake zinazosikika sana ni " THE FALLEN ANGEL" tafsiri yake ni "MALAIKA ALIYEANGUKA" utakuta kijana aliyeokoka anasikiliza na anasema hakuna shida bila kujua kuwa ni roho kamili ya kutoka kwa ibilisi na haitaji kujadiliana. Nafikiri kama umenifuatilia vizuri toka mwanzo wa kitabu utakuta kuna kicha kimoja nimezungumzia juu ya malaika muhasi aliyetupwa kutoka mbinguni Isaya 14:11,12…,Ezelieli 28:13-18, 31:8,9. hivi vitabu viwili na mistari michache itakusaidia kujua tunapozungumzia malaika aliyetupwa au aliyeanguka kutoka juu ni yupi. embu tuambatanishe na maneno ya wimbo wake,anasema,
[Verse 1:]
If I could, take a trip, to outer space
She would be the one, I will see
When I get, to heavens gate
She would welcome me with her arms, open wide, and a smile
Will shadow me brighter than the sun
She hasn't had a fair chance, so I'll give her one
Let me tell you who she is, yeah
anasema kama angeenda huko angani yeye atakuwa ndiye atakayemuona, na nikifika katika geti la mbinguni, atanikaribisha huku akitanua mikono yake na tabasamu lake liking'ara kuliko jua, anaendelea kusema, hakupewa hiyo nafasi yaani hakutendewa haki, mimi nitampa hiyo haki, anauliza je ni nani huyo? ngoja niwaambie.
biblia inazungumza kuwa Yesu pekee ndiye ambaye atatukaribiha na kutufuta machozi katika ufalme wake na si malaika aliyetupwa ambaye ni shetani! jue, hii siyo roho ya mpinga Kristo?.anasema eti tabasamu la huyo malaika aliyeanguka litang'ara kuliko jua, imeandikwa wapi? ni Yesu pekee ndiye atakayeng'ara na biblia inasema juu ya mwana kondoo ambaye ni mfalme kung'ara kule mbinguni. Hata pindi tu alipokuwa hapa duniani biblia inasema aling'ara kama jua na mavazi yake yalikua meupe kama mwangaza Mathayo 17:2
hii hapa ni korasi ya wimbo, anasema;
[Chorus:]
She's a fallen angel, sent from heaven up above
She's a fallen angel, waitin for me to love her, yeah
(Know that she's) She's a fallen angel, take your judgment off her
I know, that she's a fallen angel.
Tafsiri
yeye ni malaika aliyeanguka, kutoka juu mbinguni
yeye ni malaika aliyeanguka, akinisubiri nimpende
nafahamu kuwa yeye ndiye, muuondolee hukumu uliyompatia
ninafahamu kuwa yeye ni malaika aliyeanguka.
Je, huwa unasikiliza hizi nyimbo hasa mkristo wewe uliyeokoka, na unasema kuwa hazina shida kabisa. Wakristo wengi tunamuabudu shetani bila kufahamu, natumekuwa washabiki wa nyimbo chafu ambazo zinatukuza mambo ya ulimwengu huu ambayo ni ya uchafu na tumekubali hata kukubali ukristo uendane na kizazi kipya. Yuko wapi mchungaji ambaye atasimama na kukemea dhambi kanisani kwake, na awe pia tayari kupoteza kundi kubwa na kuponya wachache kuliko kupoteza wote kabisa?. kila wakati umuoombea mtu ugonjwa huo huo anapona na unamrudia tena, na mwingine kumuombea mtu ambaye anarudia dhambi ileile, anatubu na kurudia tena bila kujua kitu gani ambacho anasikiliza na kukiabudu. Maombia hayatamsaidia mtu kama hata tambua yeye ni nani katika ufalme wa Mungu na kuwa nuru na giza kamwe havichangamani
Ubeti wa pili;
[Verse 2:]
You know, I could Help her mend,
her broken wings,So she can fly again
But I don't, wanna lose everything that I've gained
Turnin me a selfish man (oh)
Cause without em my heart just don't go, no more (no more)
I couldn't take the pain, from watchin her fly away
So say that you'll stay,She's mine.
Tafsiri
Unajua ninaweza kumsaidia kutengeneza
bawa lake lililovunjika, ili aweze ruka tena
lakini sitaki kupoteza kila kitu nilichopata
kwakuwa mtu mbinafsi
sababu bila yeye moyo wangu umesimama kabisa
siwezi kuvumilia maumivu ya kumuona anaondoka kwangu
ndio maana nasema kwamba yeye ni wangu.
Mkristo funguka macho uone jinsi shetani anavyowatia upofu wasijue kuwa njia wanayoiendea ni ya upotevuni. Huu wimbo hauzungumzii mwanamke kama wengi wanavyofikiri, huyu anayezungumziwa hapa ni shetani, anaabudiwa na si vinginevyo. na ametumia mwanamke kama alama tu ili kukamata kizazi cha vijana, sababu uzinzi na uwasherati ndiyo nyenzo kubwa ambayo shetani anatumia kukamatia vijana.
Dada mmoja aliyekuwa mkristo mzuri na aliyeokoka vizuri tu alitoa maelezo juu ya swali hili la kusikiliza nyimbo au miziki ya dunia ya kuwa ni dhambi au si dhambi, maelezoyake kwa kifupi yalikuwa hivi,
Anasema
" mimi nimeokoka na sioni shida iliyopo katikaa kusikiliza nyimbo au miziki hii wanayoiita ya dunia, na si kwamba naitendea kazi, ila mimi napenda uimbaji tu na muziki wake na kwa kweli hauniathiri kitu chochote"
Kwanza kama mkristo nataka kukuonya kuwa usihukumu kwasababu huyu dada anaweza kuwa yuko sahihi, wala usiwadharau wengine na kuwashutumu kwa kile wanachofanya hatutaki kuwa kama mafarisayo wa kipindi cha Yesu, Luka 18:9-14 na Mathayo 7:1-5. katika mistari hii biblia haizungumzi juu ya kusikiliza muziki wa dunia ila tu inatupa muongozo. Na muongozo mwingine tunaupata katika, Wafilipi 4:8,
"Hatimaye, ndugu zangu mambo yoyote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo staha, yoyote yaliyo haki, yoyote yaliyo safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa njema; ukiwapo wema wowote, ikiwapo sifa nzuri yoyote, yatafakarini hayo."
Biblia ipo wazi kabisa, inasema kuwa 'mambo yote yaliyo ya kweli" kwa mantiki hiyo kitu ambacho unatakiwa usikilize na kukitafakari lazima kiwe katika kweli, tena yaliyo staha, na tena yaliyo ya haki, kwahiyo unaona kabisa lazima unachosikiliza lazima kijikite katika haki; yoyote yaliyo safa, mtume Paulo anaposema safi kwa maana nyingine yapo mambo yaliyo machafu na unasikiliza na kuyafakari hayo ambayo ni kinyume na Mungu; yoyote yenye kupendeza, "haleluya", mambo ambayo unatakiwa kuyasikiliza na kuyatafakari lazima yawe yenye kupendeza; yoyote yenye sifa njema, mambo gani katika muziki au nyimbo unazozisikiliza yenye sifa njema na yanakubarika na jamii nzima na biblia imeipigia muhuri kuwa ni mema? Kwahiyo unayoyasikiliza na kuyatafakari ni lazima yawe na sifa njema; na ukiwepo wema wote na sifa nzuri yoyote, Mtume Paulo anasisitiza anasema yatafakarini hayo.
Je, bado unafikiri dada huyu yuko sahihi na wala tusimuhukumu kwa kile anachokiamini na kukitenda? Ni kweli tusimuhukumu ila tunataka aifahamu kweli ya kristo ili hiyo kweli iweze kumuweka huru.
Mtumishi uliyeokoka na ambaye unamuishia Kristo na upo njiani ukiitazamia mbingu iliyoandaliwa kwa watakatifu nataka kukwambia hivi leo kuwa muziki ni roho na kila kitu chochote kilicho roho kinatambuliwa na watu wa rohoni na si watu wengine wa kawaida. Huwezi sema kuwa wimbo unapenda tu kusikiliza na haukuzuru na chochote la hasha! Kwasababu wimbo wowote unaousikia lazima uingie akilini na baadae huohuo wimbo utaingia moyoni na humo ndimo utafanya makao na baada utaanza kuimba moyoni kwasababu moyoni ndimo unapoanza kupata rithimu ya wimbo, watunga nyimbo wanaweza kuelewa kitu ninachokizungumza, kamwe huwezi ukasikiliza wimbo tu, na kukushauri kama msikilizaji wa nyimbo jifunze kufanyia kazi nyimbo unazozisikiliza ila lazima ziwe za kujenga ufalme wa Mungu na si za kubomoa.
Biblia inazungumza na kusisitiza juu ya kulinda moyo wako kuliko vitu vyote uvilindavyo maana humo ndimo zitokako chemichemi za huzima. Kwahiyo maisha yako yanategemea huwa unasikia nini na huwa unajaza nini, ukijaza maneno machafu na lazima utawaza uchafu huohuo ndiyo utakaouwaza na hakuna chemichemi za uzima tena bali chemichemi za mauti tu.Mithali 4:23
Swali ambalo ningependa ujiulize ni hili, kama mkristo unaposikiliza nyimbo au miziki ya dunia hii, je, maneno yanayozungumzwa yanaendana na kweli ambayo ipo kwenye biblia ambayo ni neno la Mungu? Je, ujumbe unaotoka ni halisi au unajenga? majibu unayo wewe mwenyewe na Mungu wako, lakini kumbuka kuwa Mungu anatuita tusienende kama mataifa wanavyoenenda, Waefeso 5:15, Mathew 10:16.
Nini unajifunza katika nyimbo unazozisikia, kwa mfano ninaweza nikakupa mfano wa nyimbo ambazo nimewahi kuzisikia na si kuzisikiliza, kwasababu nyimbo nyingi za dunia zipo kinyume na neno, mfano wa wimbo, "kamwe siwezi kukusamehe", " nimekuasamehe ila sitasahau", hizi nyimbo zinafundisha nini watoto ambao unawafungulia runinga na redio wasikilize, zinakufundisha nini wewe uliyeziweka kama mlio katika simu yako, na wewe kama mkristo unayesikiliza neno la Mungu linasema nini juu ya Msamaha, kamawakristo lazima tuwe waangalifu na tuenende katika hekima ya Kristo ili kukuza katika hekima ya Kriasto kizazi cha sasa, biblia inasema katika kitabu cha Hosea 4:6 " Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa", haisemi wanaangamia hapana wanaangamizwa, shetani mwenyewe anawaangmiza kwasababu wamekataa maarifa ya Mungu ambayo yanapatikana katika neno, unajua biblia inaendelea kusema, kwasababu watu wameyakataa maarifa basi ndiyo maana na Mungu amewasahau watoto wenu.
Kama mkristo ambaye upo katika safari ya kwenda mbinguni huwezi kupoteza muda wako kusikiliza takataka ambazo zinapotosha neno la Mungu, Mungu anatufundisha kusamehe mara saba mara sabini katika neno lake Yesu akiwa kioo chetu, Mungu anasema yeye hutusamehe dhambi kwa ajili yake mwenyewe Haleluya! Maana kutosamehe kunaleta mauti katika maisha ya mwanadamu, kwanini sasa tusikilize na kutafakari nyimbo zenye kuleta mauti?
Ukisoma biblia katika 1 Petro 5:13 na Walosai 3:16 hapo tunaona kuwa nyimbo au muziki unaleta uhai na furaha katika maisha ya mwanadamu, kwahiyo muziki ni roho kamili, kwahiyo kama nyimbo au muziki unaleta uponyaji, basi nyimbo au muziki unaleta ugonjwa na unafisha, labda kwa lugha za kiingereza tungeweza sema,
'If a song or music heals, also kills'
'Kama wimbo au muziki unauhisha, basi pia unafisha'
Siku moja nikiwa nimelala Mungu alinionesha kitu juu ya wanamuziki wakubwa na wadogo wa miziki ya dunia hasa wa kizazi cha sasa jinsi wanavyohusisha nyimbo zao na sroho za kuzimu, nikaanza kufuatilia kujua kwa jinsi gani hizi nyimbo zinahusishwa na roho za kuzimu. Natamani ufahamu kuwa wimbo wowote hauna uvuvio wa Roho Mtakatifu basi una uvuvio wa roho mtakavitu na mapepo na majini na roho chafu za kuzimu, kama nyimbo unazozisikiliza zinachochea dhambi na unajua kabisa wimbo huu aumpi Mungu utukufu ila ni mwanadamu na shetani na roho chafu kwanini usikilize? Kusikiliza na kuangalia nyimbo zenye lugha chafu na zenye kubeba ujumbe mchafu ambao upo tofauti na neno la Mungu ni hatari sana katika maisha yako ukiwa kama mkristo.
Je, ndugu msomaji unafikiri tumefanikiwa kumsaidia huyu dada ambaye haoni shida akisikiliza nyimbo za dunia na akiwa ameokoka, nafikiri tuendelee kumsaidia, Mtume Paulo anawaambia nini wakorintho?
"…basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lolote,
fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu". 1 wakorintho 10:31.
Umewafikiri kitu gain ukifanya kinampa Mungu utukufu, na maongezi gain ukiongea yanampa Mungu utukufu au mambo gain ukisikiliza yanampa Mungu utukufu, au naendeshaji maisha yako kama mkristo au naewew unalala na kuamka kama wamataifa usiju nini mapenzi ya Mungu katika maisha yako, Mungu anatutaka chochote tunachofanya lazima kimpe Mungu utukufu.
Kusudi la uimbaji na la muziki la kwanza limeshapotea kabisa, wanamuziki wa sasa wanaimba na kutunga nyimbo ili kujitafutia maslai yao wenyewe na sit u kwa mataifa tu cha ajabu na kanisa pia limejiingiza na kujichanganya huko, kanisa limekuwa ni mashindano ya biashara zaidi na kusahau kwamba kanisa lipo kwa ajili ya kuhakikisha linatunza roho za watu. Katika muziki wa sasa huwa wanaangalia nini kinalipa sana katika miziki ya sasa na ndicho wanachokiimba, kwa mfano katika miziki ya dunia kitu ambacho kinalipa sana ni nyimbo za mapenzi na ngono, nyimbo zenye lugha chafu za masengenyo na mengine yanayofanana na hayo. Je, unajua hii inaweza kusababisha nini?
"Lakini Ni hao watakao kuwa Na Mali, huanguka katika majaribu Na tanzi, Na tama nyingi zisizo Na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu. Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na imani, na kujichoma kwa maumivu mengi"1 timotheo 6:9-10
"Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wowote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu, wala aibu wala maneno ya upuzi, wala ubishi; hayo hayapendezi; bali afadhali kushukuru" Waefeso 5:3-4.
Kila mwamini au mkristo lazima ajifahamu kuwa yeye ni balozi, balozi wa nani? Balozi wa Yesu. Pinndi ulipokabidhi maisha yako kwa kristo kulitokea mgawanyiko, mgawanyiko huu ulikutoa katika ufalme wa giza kwenda ufalme wa wa nuru, kwahiyo unakuwa umetenganishwa na dunia na mifumo yake wote ingawa unaisha katika dunia hiii, Paulo anasema tupo duniani lakini sisi si wa dunia hii. Mimi nafikiri tumemsaidia dada yetu na ameelewa nini anatakiwa kufanya juu ya yote ambayo tumeyaongea.
Siku moja nilikuwa nimearikwa katika kanisa furani mjini arusha ili kufundisha juu ya kusifu na kuabudu. Ilikuwa siku ya mkesha, lakini pia kulikuwa na watoto wadogo wa kuanzia miaka mitano hadi kumi nao walikuja kukesha. Ulikuwa ni mkesha wa kusifu na kuabudu, haikuwa mara yangu ya kwanza katika kanisa hilo hasa juu ya somo la kusifu na kuabudu. kabla ya kuanza kitu chochote baada ya kufungua kwa maombi, niliuliza swali ambalo ni sehemu ya kitabu hiki, "kuna tatizo lolote mtu akiwa anasikiliza nyimbo za dunia(secular music)? majibu mengi ya hakuna shida yalitoka kwa vijana wa rika langu, na majibu ya kuwa ni tatizo yalitoka kwa watu wazima ambao walionekana kuwa wamepitwa na wakati. moja kwa moja ilipokea ufunuo wa Roho mtakatifu kuwaita watoto wadogo mbele, walikua wane wenye umri chini ya miaaka kumi. Niliwauliza huku nikitabasamu tabasamu la kutafuta ili waseme nyimbo ambazo wanasikiliza na wanazipenda kwenye luninga na radio, kila mmoja alisimulia na kanisa lilikuwa kimya likisikiliza, mambo makubwa na ya aibu watoto waliyokuwa wakisimulia, wazazi wengine walianza kuona aibu na kuangalia chini, nikasema kwa kejeli, 'hili ndilo taifa la leo'. hakikuwa kitu cha kuendelea kucheka bali kulia juu ya kizazi cha sasa, nini wajibu wa mzazi hasa wa Kristo unayemfahamu Mungu?.Kama mzazi, huwezi subiri kipaimara kikulelee mtoto,lazima uanze mwenyewe ukiwa nyumbani, komunio ya kwanza na ya pili haiwezi kukulelea mototo, ubatizo hauwezi kukulelea mtoto. ni pale tu utakapochukua hatua kuhakikisha mtoto unamlea katika maadili ya kimungu.
Kusikiliza nyimbo na miziki ya dunia kunaweza kuwa dhambi, kwasababu nyimbo zenyewe na miziki haimtukuzi Mungu,upo katika ufalme wa nuru lakini ndani yako kuna ibada ya ufalme wa giza. Kwamantiki hiyo, unaonekana katika mwili kuwa upo katika ufalme wa nuru lakini rohoni, wewe ni wa giza na shetani ana haki zote wa kukutumikisha na kukufanya wake. Nakwambia leo ufahamu ili nikusaidie mpendwa na leo ufahamu kama nilivyokwisha sema awali kuwa, nyimbo na miziki hii ya dunia huwa inakuja na roho chafu mbalimbali za kuzimu ambazo kwazo shetani anatumia kuangamiza watu na wana wa Mungu hasa rika la sisi vijana ambalo Yohana analiandikia kuwa lina nguvu na neno la Mungu limo ndani yao na kwalo wamemshinda shetani Yohana 2:14. kwanini utumie muda na fedha zakoulizopewa na Mungu kununua cds na kanda zilizobeba roho chafu kwaajili ya kujiangamiza mwenyewe na kuharibu mahusiano yako na Mungu?biblia inasema,
"Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia.Mtu akiipenda dunia wala kumpenda Baba hakumo ndani yake" 1 Yohana 2:15-17.
Hiyo makala mbona mwandishi sio wewe unasemaje kuwa ipo kwenye kitabu chako? Muandishi wa hiyo makala ya Secular music for Christian ni Rev odrick Bryson
ReplyDeleteHiyo makala mbona mwandishi sio wewe unasemaje kuwa ipo kwenye kitabu chako? Muandishi wa hiyo makala ya Secular music for Christian ni Rev odrick Bryson
ReplyDelete