JE, KUSIFU NA KUABUDU NI KARAMA?
“Kila
mwenye pumzi amsifu Bwana, Haleluya.”
Zaburi 150:6
Kama
kusifu na kuabudu ni karama basi kila mtu amepewa, lakini neno la Mungu
linasema
“…basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbal…i”Warumi
12:6
Ukisoma
tafsiri ya kiingereza ya Revised Standard Version inasema , ‘kwa kuwa tuna
karama zilizotofautiana…..’ hii ina maana kila mtu anakarama yake ingawa
wengine waweza kuwa na karama zaidi ya moja, kwa mantiki hiyo basi kusifu na
kuabudu si karama na kama unaiita karama hii ni kukwepa kuwajibika juu ya
wajibu wa kusifu na kumwabudu aliokupa yeye mwenyewe. Mara nyingi nimekuwa nikisikia katika
makanisa mbalimbali watu wakiwasifu waimbaji kuwa wanakarama ya kusifu na
kuabudu, hii siyo kweli na ni HAPANA kubwa. Tukirejea katika mstari wa Biblia
wa muongozo wetu wa kipengele hiki chenye swali ambalo linasema, Je kusifu na
kuabudu ni karama? Biblia inasema ‘kila
mwenye pumzi na amsifu Bwana’ na si kila mwenye sauti nzuri. Ukasoma tafsiri ya kiingereza inasema ‘kila
chenye pumzi|’ na kama ingekuwa kila mwenye sauti nzuri sisi wenye sauti ya
kukwaruza tusingeweza kumsifu na kumwabudu Bwana. Kwa hiyo ufike mahali utambue kama mtoto na
mtumishi wa Mungu, pumzi ambayo Mungu amekupatia ni kwa ajili ya kumsifu yeye
tu, ila yule anayesimama mbele ya umati wa watu akiimba na kuongoza kusifu na
kuabudu yeye amepewa karama ya kuongoza na si karama ya kusifu na kuabudu. Tufike
mahali tutambue ya kuwa wote tunawajibu wa kusogea mbele za Mungu kumsifu na
kumwabudu yeye kwasababu pazia la hekalu limekwisha pasuka. Matt Redman kiongozi wa kusifu na kuabudu
mmarekani anasema;
“We had
forgotten that we are all performers
of worship and
that God is the audience”
Tafsiri
yake kwa lugha ya Kiswahili ni hii ‘tumesahau kuwa sisi sote ni waabuduo na
Mungu ndiye hadhira(mtazamaji)’.
Matt
Redman alizungumza hivyo kwasababu aliliona tatizo ndani ya kanisa na katika
makongamano mbalimbali ya uimbaji kuwa wamesahau kuwa Mungu ndiye hadhira, katika
yote wanayoyafanya unapaswa kama mtumishi utambue ya kwamba Mungu unayemtumikia
au unayemwabudu na kumsifu ni Mungu mwenye wivu na hawezi kuvumilia kama
utakuwa unachukua hata sehemu ndogo ya utukufu wake. Katika maandiko mengi tulioyapitia tunaona
kuwa kumsifu na kumwabudu Mungu si karama kama wengine wangeweza kufikiri, bali
kila mmoja anawajibika kumsifu na kumwabudu Mungu hasa tukirudi katika neno
letu la muongozo katika kitabu hiki
”nao
wamwabuduo yeye imewapasa…” Yohana 4:24b,
maana
yake ni wajibu wa kila mmoja na si karama. Kwahiyo waweza kuwa Mungu amekukirimia
kuimba au kuongoza lakini si kusifu na kuabudu. hiyo ni njia ya kukwepa wajibu
na jukumu Mungu aliokupa hapa duniani. Tambua nafasi yako katika utumishi wako.